Logos Multilingual Portal

Select Language

a b c d f h i j k l m n p s t u v w z

afadhali kutokuwa na sheria kuliko kuzivunja kila siku
Ugo Foscolo
akili zote duniani hazina uwezo wa kukabiliana na aina yoyote ya kiujinga ambayo inaenea
Jean de La Fontaine
amini kila kitu unaambiwa kuhusu ulimwengu: hakuna kitu kibaya kiasi cha kutowezekana
Honoré de Balzac
ana laana askari anayewafyatua risasi wananchi wake
Simón Bolivar
anayetaka uraisi kiasi cha kupoteza miaka miwili akipanga na akifanya kampeni kwa ajili yake si mtu wa kuaminifu kwenye madaraka haya
David Broder
Asiyesoma chochote ni bora na mwenye kuelimika kuliko mtu yule asomaye Gazeti peke yake
Thomas Jefferson
asiyezuia ubaya anaamuru ufanyike
Leonardo da Vinci
bila hela na bila wasaa, fikra zinageuka ndoto ya muda mfupi ambayo haitekelei
Charles Baudelaire
busu kihalali halina thamani linayo busu lililotolewa kwa ujanja
Guy de Maupassant
chakula hatari kabisa ni keki ya arusi
James Thurber
chama cha washabiki ni kundi la watu wanaomwambia mwigizaji kwamba yeye si peke yake anapojiona wa namna fulani
Kenneth Williams
chombo kinachopungua kazi bado ni mume wenye pesa nyingi
Joey Adams
daktari ya nafsi ni mtu unayemlipa ili akuulize maswali mke wako anayokuuliza bure
Joey Adams
demokrasi ni kumchagua dikteta wako, baada ya alipomwambia mambo unafikiri unataka kuyasikia
Alan Coren
dikteta anaweza kubadili sheria siyo tabia
Jacinto Benavente y Martínez
fuateni mifano bora, yaani ile ya wanaoacha kila kitu ili wamjenge ulimwengu bora zaidi
Salvador Allende
furaha kubwa kabisa maishani ni urafiki, furaha kubwa ya urafiki ni kuwepo mtu mmoja wa kumwambia siri
Alessandro Manzoni
furaha mojawapo ya kusoma barua za zamani ni ujuzi kwamba hazitaki majibu
Lord Byron
haiba: njia ya kupata jibu la \'ndiyo\' bila ya kuuliza swali wazi
Albert Camus
haki za kibinadamu za kampuni tu zinaheshimiwa
Anónimo
hakuelewa kitu chochote kwa sababu wewe ni mtu wa mtaani; mtu wa mtaani ni mwovu, mhalifu hatari, mtu wa kawaida, mbaguzi wa rangi, mnyapara wa watumwa, hajali siasa
Pier Paolo Pasolini
hakuna kitu kinachofukarishwa kiasi ufali unavyofanya
Anónimo
hakuna kitu kinachotakiwa kubadilishwa kuliko tabia za watu wengine
Mark Twain
hakuna mtu anayesababisha madhara kuliko yule anayesaidia
Mandell Creighton
hakuna mtu anayetazama kwenye kamusi kabla ya kuzungumza
Anónimo
hali yetu ni jambo ile tunalofanya ili tugeuze hali yetu
Eduardo Galeano
hamna kitu cha muhimu sana na vitu vichache tu ni muhimu
Arthur James Balfour
hamna kitu kigumu kuliko kugundua mjinga anayenyamaa
Alonso de Ercilla y Zuñiga
hamna shaka kwamba maendeleo yanayoweza kuendelezwa ni maharibifu sana kuliko yoyote
Nicholas Georgescu-Roegen
hapana furaha bila uhuru wala uhuru bila ushujaa
Pericles
hayapo maoni ambayo mwanafalsafa asiweza kuyatoa
Marcus Tullius Cicero
historia ya wanadamu, pamoja na wokovu na laana, ina mashaka. Hatujui hata kama watawala wa maisha yetu ni sisi wenyewe
Norberto Bobbio
hofu ya upweke ni kubwa kuliko ile ya utumwa, kwa hiyo tunaoana
Cyril Connolly
hufiki mbali sana kama usipojui unakwenda wapi
Johann Wolfgang von Goethe
idadi kubwa ya wanaotawaliwa au raia wanafikiri kwamba wanataliwa kwa sababu anayetawala au mfalme anatawala; hawaelewi kwamba kwa kweli anayetawala au mfalme anatawala kwa sababu hawa ni wanaotawaliwa
Karl Marx
ilimradi watu wanakabidhi takataka, kuziuza ni faida kifedha
Dick Cavett
ilionekana kwamba duniani walikuwepo wabaya na wema tu. Wale wema walilala usingizi vizuri sana... wale wabaya walifurahia zaidi walipokuwa macho
Woody Allen
inabidi tujihadhari na mageuzi yasiyohitajika, hasa na yale yanayoongezwa na mantiki
Winston Churchill
inasikitisha kwamba wale wanaoweza kutawala nchi wanashughulika na kuendesha taksi au kukata nywele
George Burns
jambo linalofanya dunia hii mbaya ni kwamba tunajaribu kuwa na furaha na vilevile tunawazuia wengine wawe hivi hivi
Antoine de Rivarol
jicho kwa jicho, ulimwengu utakuwa na upofu
Mohandas Karamchad Gandhi
kafiri: mjini New York ni mtu asiyeamini Ukristo; mjini Istanbul ni mtu anayeamini Ukristo
Ambrose Bierce
kama vijana watakataa kibali yao hata mafia ya siri na yenye nguvu itatoweka kama njozi
Paolo Borsellino
kamusi ni kama kioo, ambamo mtu anayejua kuitumia anapata alichokikisi
Anónimo
kamusi ni ulimwengu kwa taratibu ya alfabeti
Anatole France
kanuni ya kwanza ya uandishi wa habari: kuziimarisha chuki zilizopo kuliko kuzipingana
Alexander Cockburn
katika shida kubwa sana watu wanakiamini kitu chochote
Arnold Lobel
kazi ya mtalaamu si kuwa sahihi zaidi kuliko wote, bali ni kukosea kwa sababu za kiutata zaidi
David Butler
kiasi cha watu unacho thamani yake ni sawa na kiasi cha lugha unachoongea
Carlo V
kicheko ni umbali mfupi kabisa kutoka mtu mpaka mwengine
Víctor Borge
kila kitambo chetu ni tofauti na vingine na sisi pia pia ni tofauti toka kitambo kimoja hadi kingine
Heraclitus
kila neno lilikuwa msamiati mpya siku moja
Jorge Luis Borges
kila wazo ni jambo lisilofuata tabia ya kutowaza
Paul Valéry
kinachotufananisha ni kwamba tunatofuatiana kila mmoja na mwingine
Anónimo
kisawe ni neno unalotumia usipojua kuandika neno ulilofikiria mwanzoni
Burt Bacharach
kitabu kitakuwa wokovu wa binadamu wote
Voltaire
kitu chochote kilicho akilini kilikuwa katika hisia kwanza
San Tommaso d'Aquino
kitu kinamzuia Mungu kuleta gharika la pili la maji ni kwamba la kwanza halikufaa
Nicolas de Chamfort
kivuli kinapotezwa kwenye mwanga mno... au giza mno
Moni Ovadia
kizuizi cha kuelewa kazi ya sanaa ni kutaka kuielewa
Bruno Munari
kujuta na kuanza tena tokea mwanzo - hiyo ndiyo maisha
Victor Cherbuliez
kuku jike ni njia ya yai ya kuzaa yai jingine
Samuel Butler
kumwoa mwanamke unaompenda na anayekupenda ni kushindana naye kuwa yule wa kwanza atakayeacha kumpenda mwingine
Alfred Capus
kuna nyakati, hali na mazingira ambako vurugu, na hivyo uuaji (vurugu ya juu kabisa), kwa asili inakuwa thabiti, dhahiri na uhalisia
Roberto Bolaño
kuna upeo wa hisia unaoonyesha upeo wa maisha, ambao maisha hayawezi kuendela nyuma yake. Hiyo ndiyo ajabu ya kuishi, hisia hii inafika wakati una uhai ikafika kama usahaulifu kamili wa kuwa uhai
Jack London
kupanga maktaba ni njia nyamavu ya kuhakiki
Jorge Luis Borges
kupora, kuua, kuiba, wanaita matendo hayo, kwa jina lisilo kweli, milki, na mahali ambapo wamepata jangwa wanapaita amani
Tacitus
kusema urafiki ni kusema uelewano kamili, kuamiana kwa mara moja na ukumbukaji wa kudumu; kwa neno jingine, uaminifu
Gabriela Mistral
kusoma ni kutafsiri, kwa sababu uzoefu wa watu wawili haufanani. Msomaji mbaya ni kama mfasiri mbaya. Unapojifunza kusoma, silika yako ni muhimu zaidi kuliko ujuzi
Wystan Hugh Auden
kutaka mambo yale yale na kutotaka mambo yale yale, hicho ndicho urafiki wa kweli
Caius Sallustius Crispus
kutoka mambo yote ya uhakika, jambo la uhakika zaidi kuliko yote ni shaka
Bertolt Brecht
kutotaka ni kama kumiliki
Lucius Annaeus Seneca
kuwa mjana na kutokuwa mwanapinduzi ni mkingamo wa kibiolojia
Salvador Allende
kuwaitikia ndio watu wote na kwa vitu vyo vyote kunafanana na kutowepo
Tahar Ben Jelloun
kwa hakika amani kabisa kati ya mume na mke ni kuachana
Lord Chesterfield
kwa kawaida, mambo mabaya yatendwayo kwa kisingizio kuwa yanatakiwa na maendeleo, si maendeleo yoyote, bali ni mabaya tu
Russell Baker
kwa nini niwajali kizazi cha baadaye, hawa walinisaidia vipi?
Groucho Marx
kwa wanawake wengi njia fupi ya kufika ubora ni upole
François Mauriac
kweli inawezekana kumsamehe mtu mjinga wa saa moja tu, wakati wako wengi wasioacha ujinga hata saa moja ya maisha yao
Francisco de Quevedo y Villegas
kwenye mafanikio marafiki wanatujua, kwenye taabu sisi tunawajua marafiki
John Churton Collins
kwenye mwanga wengi kivuli cheusi sana
Johann Wolfgang von Goethe
labda sikuhizi lengo letu si kugundua hali tusiyokuwa nayo, bali kuikataa ile tunayo
Michel Foucault
laiti ingekuwa rahisi kugundua ukweli kiasi ilivyo rahisi kufichua uwongo
Marcus Tullius Cicero
lalamiko la zamani kwamba elimu ya wote inakusudiwa kwa wanao umri wa miaka kumi na mmoja ni uongo mkubwa. Umri maalumu kwa desturi ni wa miaka kumi na minne
Robert Christgau
lugha ni sanaa isiyokusudia ya watu wengi kwa pamoja, tokeo la ubunifu wa vizazi vingi
Edward Sapir
macho mazuri ni yale yanayokuangalia kwa upole
Coco Chanel
maendeleo ni kama nyota iliyokufa: tunazidi kuona mwanga wake hata kama imezimika zamani sana na kwa daima
Gilbert Rist
maisha bila ujasiri wa kuyapigania yana maana gani?
Giuseppe Fava
maisha ni hospitali ambamo kila mgonjwa anataka kuhama kitandani
Charles Baudelaire
maisha yetu yanaisha tunaponyamaa kuhusu mambo muhimu
Martin Luther King
malezi ni njia ya kuwarithisha watoto dosari za wazazi wao
Armand Carrel
maneno ni muhimu kama ni machache
Lalla Romano
maneno ya zamani na mafupi, \'ndiyo\' na \'siyo\', ndiyo maneno yanayostahili yajaliwe kuliko yote
Pythagoras
matakwa ya kwanza ya kiongozi wa taifa ni awe mzito wa kuelewa. Hiyo haipatiwi kwa urahisi
Dean Acheson
matumaini ya mwisho ni kuamini kwamba matumaini yote yamepotezwa
Maurice Chapelan
mawakili tu hawaadhibiwa wasipojua sheria
Jeremy Bentham
mawakili tu ni wahalifu wanaochagua mahakimu yao miongoni mwao
Charles Caleb Colton
mbezi: baa anayeona mambo yaliyo siyo yanavyotakiwa yawe.
Ambrose Bierce
mchezo wa mpira uwe huru kutoka maduka ya madawa na ofisi za kifedha
Zdenek Zeman
mgonjwa wa wasiwasi ni mtu anayejua sehemu ndogo ya mambo yanayoendelea
William S. Burroughs
mikutano ya upunguzaji wa silaha za vita ni mazoezi ya kuzuia moto ya wapendao kuchoma moto
John Osborne
mipaka ya lugha yangu ni mipaka ya dunia yangu
Ludwig Wittgenstein
mkijiamini mnawaaminiwa na wengine
Johann Wolfgang von Goethe
mtaalamu ni mtu aliyefanya makosa yote yanayowezekana kufanyiwa katika fani ndogo sana
Niels Bohr
mtu aliye mbingwa wa lugha yake hawezi kuwa mbingwa wa lugha nyingine
George Bernard Shaw
mtumwa ni mtu anayemsubiri mtu anayeweza kumweka huru
Ezra Pound
Mungu hawezi kubadili siku za zamani, kwa hiyo lazima afumbie macho kuwepo kwa wanahistoria
Samuel Butler
mustakabali tu ni mali wakuu wanayowatoa watumwa wake kwa nia
Albert Camus
mwanasiasa hujali uchanguzi ujao, kiongozi wa taifa hujali kizazi kijacho
Otto von Bismarck
mwanasiasa ni mwanasarakasi: hayumbi kwa kusema kinyume cha anayofanya
Maurice Barrès
mwigizaji ni mtu ambaye usipokuwa kumzungumzia kuhusu yake hakusikilizi
Marlon Brando
napenda sana vyama vya siasa: ndipo hapa tu ambapo watu hawaongei kuhusu siasa
Oscar Wilde
nchi isiyo na filamu ionyeshayo hali halisi yake ni kama familia isiyo na kitabu cha picha
Patricio Guzmán
ndoa ni kama uyoga: tunapogundua ubora au ubaya wake tumechelewa mno
Woody Allen
ndoa: jamii yenye bwana mmoja, bibi mmoja na watumwa wawili, ambapo wote ni wawili tu
Ambrose Bierce
nguvu ya tabia ni mkubwa
Marcus Tullius Cicero
nilipokuwa mtoto niliweza kukumbuka mambo yote, yaliyotokea pamoja na yale ambayo hayakutokea
Mark Twain
ningependa kwamba shahada ya kifo ya kila mtu iwe na lugha ile ile ya shahada yake ya kuzaliwa
Bertolt Brecht
ningesema ninayoyafikiri kweli, ningefungwa rumande au kutengwa katika nyumba ya wendawazimu. Wacha! Nina hakika ingekuwa hivi hivi kwa wowote
Roberto Bolaño
nini itafikia mwisho wake kwanza: hewa au mafuta?
Anónimo
nini kizuri zaidi kwa watu kuliko lugha ya wazee wao?
Johann Gottfried von Herder
nini kuiba benki kulingana na kulianzisha
Bertolt Brecht
njia halisi ya kutunza afya yake ni kula chakula usichotaka, kunywa kinywaji unsichopenda, kufanya mambo usingeyafanya
Mark Twain
nuru ya Mungu inawatia wanadamu upofu badala ya mwanga
Patrick Emin
pamoja na kila lugha inayokufa taswira ya mtu inapotea
Octavio Paz
sayansi hufaa kumthibitisha uvumbuzi wa silika
Jean Cocteau
sehemu bora kuliko zote za riwaya ni onyo kwamba wahusika wote ni wa kubunika
Franklin Pierce Adams
siasa na adili zimeundwa kwa ajili ya watu wasio na matazamio wala ukubwa. Wale wanao ukubwa hawahusiki na siasa
Albert Camus
siasa ni taaluma ya kuwazuia watu wajishughulikie na mambo yanayowahusika
Paul Valéry
siasa ni ustadi wa kutafuta matatizo, kuyapata, kuyatambua vibaya na kutumia mbinu mbaya ya kuyatatua
Groucho Marx
sifikiri inanilazimu kuamini kwamba yule Mungu anayetujalia uelewa, hisia na akili ndiye anayekusudia tusizitumie
Galileo Galilei
sigara ni mfano halisi wa furaha halisi. Ni bora kabisa ikamfanya mtu asirishike. Nini zaidi?
Oscar Wilde
siku za baadaye za watoto ni leo, kesho zitakwisha
Gabriela Mistral
silika ya kuua, kama silika nyingine, ni sehemu ya utu. Ziko pamoja: mtu na kifo, mtu na ukatili, mtu na damu. Haifurahishi, lakini hii ni hali halisi
Roberto Bolaño
sinema, kama michoro, inaonyesha kisichoonekana
Jean-Luc Godard
soko ni mahali ambapo watu wanaweza kudanganyana
Anacharsis
tabasamu: meno yako si kwa ajili ya kulia au kung\'atia tu
Man Ray
tafsiri, kama wake, zinapovutia mara chache tu ni aminifu
Roy Campbell
takwimu juu ya hali ya akili zinaonyesha kwamba mmoja kati ya wamarekani ana aina moja ya ugonja wa akilini. Uwachunguze marafiki yako watatu. Wakiwa wazima, basi wewe ndiye yule mgonjwa
Rita Mae Brown
tatizo la kuheshimu muda ni kwamba hayupo mtu yeyote anayeweza kukuthamini
Franklin P. Jones
tatizo la wanadamu ni kwamba wajinga wana uhakika kabisa, bali wenye akili wana mashaka mengi
Bertrand Russell
televisheni inavutia zaidi kuliko watu wengine; isingekuwa hivyo tungeweka watu kwenye pembe za chumba
Alan Coren
tendo la kisasi kubwa kuliko yote la mwanamke ni kuendelea kuwa mwaminifu kwa mtu
Jacques-Bénigne Bossuet
thamani halisi ya mtu inaonyeshwa na uwezo wake wa kupata uhuru kutoka yeye mwenyewe
Albert Einstein
tofauti kati ya demokrasia na udikteta ni kwamba kwenye demokrasia unapiga kura kwanza, unaamrishwa baadaye; kwenye udikteta hautakiwa kupoteza wakati wako kwa kupiga kura
Charles Bukowski
tukitaka kugeuza mambo lazima kushika mabenki na kulipisha televisheni. Hauko utatuzi wa kimapinduzi mwingine
Luciano Bianciardi
tulieneza sarakasi, bali hatujaeneza mkate
Anónimo
tunajua kwamba mtu anaweza kusoma Goethe au Ritke jioni, kucheza muziki wa Back au Schubert, na asubuhi yake kufanya kazi kule Auschwitz
George Steiner
tunaweza kusema kwamba uhuru ni kitu kisicho dhahiri, lakini kutokuwepo kwake ni dhahiri sana
Rodrigo Rey Rosa
tunaweza kuwagawa binadamu kulingana na aina tatu: wale waliochushwa kabisa, wale aliochukizwa kabisa na wale waliohangaishwa kabisa
Winston Churchill
tuungane, hatutashindika
Simon Bolivar
uaminifu upo kwenye upenzi wenye nguvu zaidi ya silika
Paul Carvel
uamuzi wa kikristo wa kutafuta ubaya na uovu wa ulimwengu, mwishoni umefanya ulimwengu mbaya na mbovu
Friedrich Wilhelm Nietzsche
ubinafsi si kuishi kama tunavyopenda, bali kuwafanya wengine waishi tunavyopenda
Oscar Wilde
ubunifu si kitu kingine cha tokeo la kumbukumbu yetu
Pierre Bonnard
udhanifu ni safi, lakini unapokaribia uhalisia gharama yake inakuwa ya juu mno
William F. Buckley
ufahari mzima wa wanadamu umo ndani ya punje ya ngano
José Martí
ujuzi unaendelea kwa sababu tunaweza kujitegemea wataalamu wa zamani waliotutangulia
Margherita Hack
ukiona mababa wa kawaida, si bahati mbaya kutokuwa na baba; vilevile ukiona watoto wa kawaida si bahati mbaya sana kutokuwa na watoto
Lord Chesterfield
ukiota utakuwa huru rohoni, ukipigana utakuwa huru maishani
Ernesto Che Guevara
ukitaka picha ya mustakabali fikiria buti linalomkanyaga uso la mtu... milele
George Orwell
ukivumilika kitu, hicho kitastahimilika na kabla haijawamuda mrefu kitakuwa cha kawaida
Israel Zangwill
ukweli halisi umo mwenye silika
Anatole France
unajifunza fani ya ushindi kutoka ushinde
Simon Bolivar
unapoona bepari akiruka chini kupitia dirisha umfuate, pale chini patakuwepo fedha
Robespierre
unapotambua upo upande wa wengi, afadhali usimame ukatafakari
Mark Twain
unataka wengi wakusaidie? Jaribu kutokuwa na haja za msaada.
Alessandro Manzoni
unaweza kuwa na lugha bila pesa, mali, utawala au ndoa, bali huwezi kuwa na pesa, mali, utawala au ndoa bila lugha
John Searle
uongo tu unahitaji kutegemezwa na serikali, ukweli unajitegemea peke yake
Thomas Jefferson
upendo huo wa vitabu ndio ulinifanya mjinga wa kupita wote
Louise Brooks
upya una umri ule ule wa dunia
Jacques Prévert
usiwe na choyo: uwaheshimu wenye choyo
Stanislaw Jerzy Lec
utoto unapokufa, maiti yake inaitwa wazima wakaingia jamii, jina moja la jahanamu. Hiyo ndiyo sababu tunawaogopa watoto, hata tukiwapenda. Wao wanatuonyesha kiwango cha uozo wetu
Brian Aldiss
uwe mpumbavu lakini kwa shauku
Colette
uwe na macho wazi kabla ya ndoa, nusu wazi baadaye
Benjamin Franklin
vita ni kutafuta amani kwa umwagikaji wa damu, bali amini ni kuendelea mapigano bila umwagikaji wa damu
Anonimo
vitabu vina kiburi chake: ukivikopesha havirudi tena
Theodor Fontane
waandishi habari hawaamini uwongo unaosemwa na wanasiasa, lakini wanaurudia: vibaya zaidi!
Coluche
wafasiri ni kama wachoraji: waweza kuboresha nakala, lakini lazima ifanane na asili yake
Elie Fréron
wakati Dk Johnson alipoeleza maana ya neno la \'uzalendo\' kama kimbilio cha mwisho cha waovu, alisahau sifa kubwa za msemi wa \'urekebishaji sheria\'
Roscoe Conkling
wakati fulani nilisoma kamusi tangu mwanzo mpaka mwisho, nilifikiri ilikuwa riwaya nzuri kuhusu kila kitu
Ophelia
wakati mtu anapojidai kufahamu furaha, bila shaka ameshaipoteza
Maurice Maeterlinck
wakati mwanasayansi mashuhuri, lakini mzee, anaposema kwamba kitu fulani kinawezekana, yumkini yuko sahihi; anaposema kwamba kitu fulani hakiwezekani, inawezekana sana kwamba anakosea kabisa
Arthur C. Clarke
wakili ni muungwana anayeokoa mali yako kutoka adui yako akaichukua mwenyewe
Henry Brougham
wale wasiofikiria ingekuwa afadhali wachunguze chuki zao mara kwa mara
Luther Burbank
wanadamu wana silaha inayofaa kwa kweli kabisa: kicheko
Mark Twain
wanataka vita, lakini sisi hatuwaacha katika amani
José Saramago
wanyama wote wana roho, isipokuwa watu kadhaa
Anónimo
watoto kamwe hawawasikii wakubwa wao, lakini kamwe hawajashindwa kuwaiga
James Baldwin
watu hawasemi uongo kama kabla ya uchaguzi, wakati wa vita, baada ya uwindaji
Otto von Bismarck
watu wanaulizwa maoni mara kiasi kwamba sasa hawana tena maoni
Jean Baudrillard
watu wengi hawaogelei kabla ya kujifunza kuogelea
Hermann Hesse
wewe ni Bi. Smith, mtoto wa mwenyebenki tajiri Smith, sivyo? Sivyo? Unisamehe, kwa muda mfupi nilifikiri nilishikwa na upendo kwako
Groucho Marx
wezi huheshimu mali; wanataka mali ziwe zao ili waweze kuziheshimu vizuri zaidi
Gilbert Keith Chesterton
zipo aina mbili za televisheni, ile wenye akili inayolea raia wasiotawaliwa kwa urahisi, ile ya wapumbavu inayolea raia wanaotawaliwa kwa urahisi
Jean Guéhenno